MATOKEO YA KURA YA KUPITISHA BAJETI 2017/18 BUNGENI- 


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 kwa asilimia 73.
Bajeti hiyo ambayo ni Shilingi Trilion 31 iliwasilishwa Juni 8 mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.
Akitangaza matokeo ya upitishwaji wa Bajeti hiyo, Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah alisema idadi ya wabunge wote waliokuwepo 356 na kwamba waliopiga kura za ndiyo ni 260 huku kura za hapana zikiwa 95.
“Kwa matokeo haya,Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 kwa kupigiwa kura na wabunge 260 sawa na asilimia 73,” alisema Dkt. Kashililah.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai aliipongeza Serikali kwa niaba ya Bunge pamoja mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na watendaji wote waliofanikisha mchakato huo.
“Mchakato huu umepitia katika hatua nyingi, ninawaomba wabunge tuendelee kushiriki pia katika utekelezaji wake,” alisema.
Alisema Bajeti ya mwaka huu ni ya mfano kwa kuwa Serikali imewasikiliza wananchi na kwamba hata hivyo matatizo ya nchi hayawezi kumalizika kwa bajeti moja.
“Kwa hiyo tutaendelea kusema na kuishauri Serikali ili nchi yetu iendelee kupiga hatua,” alisema.

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .