Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye ameitaka Serikali ya awamu ya tano kukivumilia


Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye ameitaka Serikali ya awamu ya tano kukivumilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kwani kinafanya kazi zake kama CCM hivyo amesema ni bora kikaachwa huru.
Ameyasema hayo jana mara baada ya kukamatwa kwa Meya wa Ubungo, Jacob Steven wakati wa maandalizi ya ziara ya kutembembelea Manispaa hiyo kwaajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema kuwa Serikali haitafanikiwa kama itaendelea kukizuia chama hicho kufanya shughuli zake mbalimbali za kichama kwani kila chama kina haki ya kikatiba ya kufanya shughuli zake.
“Kwa jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani wataleta vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye kazi zao hapa hakuna siasa zozote tunazofanya, tunakagua miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea kwenye halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na sisi tunataka kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale ambayo CHADEMA imewaagiza kufanya katika Ilani yake, na miradi hii ni kwa wananchi wote,”amesema Sumaye.
Hata hivyo, ameongeza kuwa hilo si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM huku akimtolea mfano Pole Pole anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna tatizo ila inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza
mapambano
#dar24

Comments


Popular posts from this blog

Mambo 10 ukiyazingatia wewe ni mke bora katika ndoa

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

CHADEMA yafunguka Hospitali aliolaza Tundu Lissu

Wasanii vinara kwa ushirikina watajwa

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .

Tanzania inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki

Aliyemuoa mwalimu wake ataka mahakama iwatenganishe bila sababu.

mimi nipo sex Lulu diva

Shamsa amuoneaa wivu Odama