wanafunzi 10 wafutiwa matokeo kidato cha sita kwa udanganyifu


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde
Zanzibar. Wakati matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai 15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.
Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.
Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .