Diego Costa na Antonio Conte, ndani ya vita nzito



Sasa ni mwendo wa vijembe tu kati ya Diego Costa na Antonio Conte, huyu anasema hiki na yule anamcheka huyu lakini yote inaweka wazi kwamba Costa na Conte hawapo katika mahusiano mazuri kwa sasa.
Wiki iliyopita kocha Antonio Conte aliulizwa kuhusu maneno ya Diego Costa kwamba msimu uliopita timu ya Chelsea iliishi naye kama mkosaji, Conte badala ya kujibu swali hilo alibaki tu kucheka jambo ambalo lilitafsiriwa tofauti.
Sasa Diego Costa naye ameibuka upya akikumbushia ujumbe mfupi wa maneno aliotumiwa na Antonio Conte na kusisitiza kwamba ujumbe huo ulimfanya aelewe Antonio Conte ni mtu wa namna gani.
“Ujumbe wake ilikuwa kipindi cha ajabu sana na ilinipa picha kufahamu kwamba ni mtu wa namna gani na mimi niliwaza ni ukosefu wa heshima” alisema Diego Costa.
Diego Costa amesema yeye binafsi mara nyingi amekuwa akiongea na bodi ya timu kama akiwa ana shida ya kukutana na kocha, Costa amesisitiza yeye huwa hatumi message kwa kuwa anaona sio nidhamu kufanya hivyo.
Diego Costa yuko mbioni kurudi katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na amesisitiza ya kwamba tayari ameshafanya maamuzi hatarudi

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

hii ndio furaha ya Diamond na zari

SI KWELI KUWA MAREHEMU FRANCIS KANYASU NDIYE ALIYEBUNI NEMBO YA TAIFA