Msanii wa filamu Johari aweka wazi mahusiano yake na Ray kigosi


Msanii nguli wa filamu ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu Bi. Blandina Chagula, ameweka wazi mahusiano yake na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi, ambaye wanamiliki kampuni moja ya filamu.
Akizungumza na mwandishi wetu Johari amesema hawezi kuvunja mahusiano yake na Ray ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji mwengine Chuchu Hansa, kwani wana miliki kampuni kwa pamoja.
"Mimi na Ray tunafanya kazi, kwa hiyo kuachana nae ni vigumu, naacaha nae kivipi sasa wakati wote tunamiliki kampuni ya RJ? Yule ni mkurugenzo mwenzangu kwa hiyo sio rahisi kuvunja uhusiano wetu", alisema JOhari.
Pia Johari amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani anatarajia kuwapakulia kazi mpya, ambayo itakuwa inawaletea yule Johari waliyemzoea kwenye filamu zake zenye ubora wa hali ya juu.
"Unajua mi siwezi kuacha anaa kwa sababu sanaa ni maisha yangu, siku si nyingi ntatoa kazi mpya hii kazi haina kustaafu,m na sasa hivi wale wasanii wakongwe karibia wengi tunajipanga kurudi kwenye game, kwa hiyo watu wakae mkao wa kula", alisema Johari.
Hivi sasa Johari amekuwa kimya kwa muda mrefu kuonekana kwenye kamera, na badala yake amekuwa mtu ambaye anakaa nyuma ya kamera kwenye utengenezaji wa filamu nyingi zinazotengenezwa na kampuni ya RJ.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu