Sina uadui na Korea Kaskazini Marekani


Serikali ya Marekani kupitia Waziri wake wa Mashauriano ya Kigeni Rex Tillerson, imesema haitaki mabadiliko ya utawala Katika Korea Kaskazini. Makao makuu ya wizara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon, yametoa taarifa za hivi karibuni juu ya hatua za kijeshi.
Majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini yamesababisha hofu kubwa juu ya tishio la serikali ya Korea Kaskazini dhidi ya Marekani, huku ikizingatiwa kwa haja ya kuzuwia shambulio lolote nchini Marekani.
Hata hivyo hofu inaendelea kutanda kuhusu mpango wa silaha wa Korea Kaskazini.
Bwana Tillerson amesema Marekani haitaki mabadiliko ya utawala na kuongeza kuwa lengo ni kufanya mazungumzo, lakini ambayo hayana msingi kwamba Korea Kaskazini inaweza kuendelea kutunza silaha zake za nuklia
" Hatutaki mabadiliko ya utawala, hatulengi kuuangusha utawala, hatutaki kuharakisha muungano wa eneo la Peninsula, hatutaki sababu ya kutuma wanajeshi wetu kwenye eneo lenu ," alisema RexTillerson.
Bw Tillerson alibaini kwamba Marekani ilitaka mazungumzo wakati mmoja na Korea Kaskazini.
Seneta kutoka chama cha Republican alisikika akisema kuwa rais Trump alihisi kuanza vita na Korea kaskazini ni chaguo jema.
Korea Kaskazini inasema kuwa jaribio lake la hivi karibuni la makombora linaweza kushambulia magharibi mwa Marekani.
Na Rfi

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu