Maswali 10 yakujibu dereva wa Lissu

kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto aliamuru Jeshi la Polisi kumsaka dereva aliyekuwa akimuendesha Mbunge Tudu Lissu pindi shambuluio lilipokuwa likitokea ili kumfanyia mahojiano na uchunguzi wa awali.
Ambapo maswali kwaajili ya mahojiano na dereva huyo yalifafanuliwa kama ifuatavyo;
1. Kuna vitu gani vya Lissu amevichukua hadi sasa hajavisalimisha?.
2. Amekuwa dereva wa Lissu kwa muda gani, kabla ya kutokea kwa tukio hilo la kupigwa risasi?.
3. Nani alimuunganisha dereva huyo na Mbunge wa Singida Mahariki CHAEDEMA Tundu Lissu?.
4. Kabla ya kuwa dereva wa Lissu amewahi kumuendesha kiongozi mwingine yeyote?.
5. Licha ya kudaiwa Lissu alipigwa risasi zaidi ya 25, lakini hakuna hata moja iliyompata dereva katika hali ya kawaida hilo haliwezekani?.
6. Alidai kutambua mapema kuna gari linawafuatilia kwa nini hakutoa taarifa na tahadhari gani alichukua?.
7. Kwa nini baada ya kuona kuna gari linawafuatilia hakwenda kituo chochote cha polisi?.
8. Mpaka sasa hajajisalimisha kwa vyombo vya ulinzi na usalama, je jambo hili si kiashiria kwamba kuna anachohofia?.
9. Kwa nini baada ya tukio aliamua kwenda mafichoni na si kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama?.
10. Katika hali ya kawaida gari alilokuwa analitumia Lissu limetengenezwa katika namna bora zaidi ya kukimbia ukilinganisha na Nissan waliyokuwa nayo ho wavanizi, iweje alishindwa kuwakimbia?

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu