Msuva amejiunga na timu hiyo Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga, lakini sasa ukitaka kumpata, Waarabu wanamthaminisha kwa euro 475,000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3. Mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao sita kwenye ligi ya nchi hiyo huku akifunga mabao manne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali ya mabao hayo, Msuva amefanikiwa kucheza mechi 16 za ligi na moja ikiwa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliofanya thamani yake kuongezeka. Kwa mujibu wa mtandao mmoja maarufu nchini Morocco ambao unahusika kutoa taarifa za thamani ya wachezaji, dau la Msuva sasa ni euro 475,000. Dau hilo ambalo limeonekana kupanda kwa Msuva, pia unaweza kusajili kikosi kizima cha Simba ambacho kilitajwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 1.3. Kuongezeka kwa thamani ya mshambuliaji huyo, kumetokana na kuonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi ya Morocco tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Yanga msimu uliopita ambao aliondoka akiwa ni mfungaj...