Posts

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe ameyasema haya

Image
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali, atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi. Akiwajibu wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho. “Sitaki na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto Kabwe. Zitto Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria mpaka ndoto zao zilipotimia. “Kagame alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa, Meles mpiganaji dhidi...

Ofisi ya wakili Fatma Karume na Masha yawaka moto

Image
Ofisi hiyo iliyoungua moto inamilikiwa wakili Fatma Karume pamoja na Lawrence Masha, aidha baadhi ya watu wamejitokeza na kulaani kitendo hicho. Hata hivyo kikosi cha Upelelezi cha Polisi kinaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo kilichopelekea ofisi hiyo kuweza kuwaka moto majira ya usi ku wa kuamkia 26 Agosti 2017.

Barcelona sasa yawa moto baada ya hili

Image
Ni siku 21 baada ya staa wa kimataifa wa Brazil  aliyekuwa anaichezea  FC Barcelona   Neymar  aamue kuihama club hiyo na kujiunga na  Paris Saint Germain  ya  Ufaransa  kwa rekodi ya dunia ya pound milioni 199, leo  FC Barcelona  wamesajili mbadala wake. FC Barcelona  ambao walikuwa wamelenga kumsajili mbrazil  Philippe Coutinho   kutoka Liverpool  au  Ousmane Dembélé  kama chaguo lao la pili kama wakimkosa Coutinho ,  leo August 25 wamefanikiwa kumsajili  Ousmane Dembélé  kwa uhamisho wa pound milioni 96 ambazo zinaweza kuongezeka hadi kufikia pound milioni 136. Kwa uhamisho huo sasa  Ousmane Dembélé  mwenye umri wa miaka 20   ndio anakuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya  Neymar , Dembele  amesajiliwa akitokea  Borussia Dortmund  ya  Ujerumani,  maamuzi hayo ya  FC Barcelona  yamekuja baada ya kuka...

Magazeti ya Tanzania leo August 26 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews

Image
Add caption Ni ahabari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 26  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

Mwanamke anahitaji vitu hivi kutoka kwa mwanamume

Image
Kutatuliwa Matatizo Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke. Kubembelezwa Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Kuwa chaguo namba moja Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa. Wanapenda watangulizwe katika mapenzi ...

Makonda apokea Pikipiki 10 za Askari wa usalama barabarani

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaa jili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China. Hatua hiyo inakuja baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwa ajili ya kuongoza misafara ya viongozi, Misiba na kuwahisha hospitali wagonjwa waliozidiwa.

Diamond mchokozi amepost hiki baada ya Alikiba kuachia wimbo wake

Image
Muda mfupi baada ya mwimbaji staa Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ leo August 25, 2017, staa mwingine wa Bongofleva kutokea WCB, Diamond Platnumz amepost picha kwenye Instagram. Diamond amepost picha ya mtu akicheka kitu kilichowafanya mashabiki kuunganisha matukio wakidai huwenda picha hiyo ni ujumbe baada ya kuusikia wimbo wa Alikiba.

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 25.08.2017

Image
Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kwa pauni milioni 35 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi ijayo. (Daily Telegraph) Chelsea wananajaribu kufanikisha usajili wa pauni milioni 15 wa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, ambaye alicheza chini ya Antonio Conte, Juventus. (Daily Telegraph) Juventus wamewasiliana na Chelsea kumuulizia beki wa kati Gary Cahill. (Sun) Manchester City wamekata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 150. (Sun) Manchester City watapanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (Times) Mchezaji wa Monaco Thomas Lemar amesema angependa zaidi kujiunga na Manchester United badala ya Arsenal. (Duncan Castles) Zlatan Ibrahimovic amekubali kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia hamsini mwezi Januari, baada ya kusaini tena kubakia Old Trafford. (The Sun) Barcelona wamekubaliana mkataba wa pauni mili...

Droo ya Kombe la Ligi- EFL Cup

Image
Mabingwa watetezi wa Kombe la EFL Manchester United wataanza kutetea taji lao kwa kuwakaribisha Burton Albion kwenye dimba la Old Trafford. Liverpool watakuwa ugenini kupambana na Leicester City. Manchester City watakaribishwa na West Brom, huku Arsenal wakicheza na Doncaster Rovers. Nottingham Forest walioichapa Newcastle United jana, watakwenda Darajani kukutana na Chelsea. Mechi za kwanza za Kombe la EFL zitachezwa katika wiki ya Septemba 18. Msimu huu Kombe la Ligi litajulikana kama Kombe la Carabao (Carabao Cup) kutokana na wadhamini wa michuano hii. Droo kamili ni kama ifuatavyo: West Bromwich Albion v Manchester City Everton v Sunderland Leicester City v Liverpool Manchester United v Burton Albion Brentford v Norwich City Wolverhampton Wanderers v Bristol Rovers Burnley v Leeds Arsenal v Doncaster Rovers Bristol City v Stoke City Reading v Swansea City Aston Villa v Middlesbrough Chelsea v Nottingham Forest West Ham United v Bolton Wanderer...

Rais Magufuli Acharuka

Image
Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema anataka watu wanaokula rushwa wengi wao wafungwe kwani watu hao wanasababisha watu wakose barabara, madawa na kukosa maendeleo kutokana na watu kula rushwa. Rais Magufuli amesema hayo jana wakati akimuapisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kumtaka afanye kazi kuhakikisha rushwa inakomeshwa. "Umepewa hilo jukumu kalisimamie na tunaimani kubwa kwamba utakwenda kulisimamia kwa uadilifu mkubwa ukishirikiana na wenzako waliopo pale nina uhakika mtafanya kazi kubwa hasa katika suala la uchunguzi, nataka wala rushwa wengi wafungwe hilo mimi nalitaka najua maneno kama haya hawayataki watu kuyasikia, nataka wala rushwa wengi wafungwe" alisisitiza Rais Magufuli Aidha Rais Magufuli anasema kuwa wakifungwa wala rushwa wengi hivyo rushwa itakuwa imekwisha kwa sababu wale walaji wote watakuwa magerezani na kudai hao ndiyo wamekuwa walimu wa wala rushwa, lakini Rais ...

Kenya Wabunge na Maseneta wapya kuapishwa wiki ijayo

Image
Bunge la Kenya lina wabunge 349 huku Maseneta wakiwa 67, ikiwa ni pamoja na wale walioteuliwa na vyama mbalimbali vya siasa. Pindi tu baada ya kuapishwa, bunge la kitaifa na lile la Senate litawachagua Maspika na Manaibu wao, na bunge sasa kuanza kazi yake rasmi baada ya wiki moja. Wabunge na Maseneta wataapishwa siku moja tu kabla ya Mahakama ya Juu, kutoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta. Mbali na suala hilo, Wakenya wamewashtumu wabunge waliochagulia kwa kukakaa pendekezo la kuwapunguzia mshahara. Wabunge nchini Kenya wamekuwa wakilipwa Dola za Marekani 7,200 kila mwezi na mwezi Juni mwaka huu, Tume ya kusawazisha mishahara iliamua kupunguza mishahara yao kwa asilimia 15. Wabunge wa zamani waliochaguliwa tena na wale wa sasa wamelaani hatua hii na kusema,, hawatapitisha mapendekezo ya Tume hiyo. Wanasiasa hao wanasema hatua ya Tume hiyo inalenga kuwanyanyasa.

Magazeti ya Tanzania leo August 25 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews

Image
Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 25  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.