Watu kumi na mmoja wauawa katika shambulio

Askari wasiopungua tisa na raia wawili walikatwa vichwa siku ya Jumatano nchini Libya katika shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State dhidi ya ngome ya majeshi yanayomtii Marshal Khalifa Haftar.
Shambulio hilo lilifanyika mapema alafajiri katika eneo la al-Joufra, kilomita 500 kusini mwa Tripoli, kwa mujibu wa Kanali Ahmed al-Mesmari, msemaji wa kundi la wapiganaji wa NLA linalomtii Marshal Haftar.
Siku ya Jumatano alasiri, kundi la Islamic state lilidai kutekeleza shambulio hilo katika taarifa iliyotolewa na shirika lake la propaganda la Qama. Anadai kuwa aliua na kujeruhiwa "wanamgambo 21 wa Haftar" katika shambulio la "wapiganaji wa IS" kusini mwa al-Joufra.
Wapiganaji wa kundi la NLA walikua walidhibiti eneo hilo mapema mwezi wa Juni.
Lakini mapigano yanaendelea kati ya makambi mawili karibu na wilaya ya Soug al-Hout.

  Na Rfi

Comments


Popular posts from this blog

Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini waimarika

harakati za ndesamburo na utajiri wake hizihapa

ACACIA wapinga vikali matokeo ya kamati ya pili ya Rais

IsraelIsrael yasalimu

mimi nipo sex Lulu diva

Real madrid mabingwa tena UEFA

Rais Zuma akiri kunusurika kuuawa kwa sumu

Hatua 10 Muhimi za Kumchagua Mchumba Mtakae Funga Ndo. a tzaama SOMA NA SHARE HII