Posts

Showing posts from June, 2017

Magazeti ya Tanzania leo June 30, 2017, Udaku, Michezo na Hardnews

Image
   Good Morning mtu wa nguvu, leo ni May 30  2017  na kama ilivyo kawaida yangu ya kila siku alfajiri nimekusogezea habari kubwa kwenye Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya  Udaku ,  Hardnews  na  Michezo  ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

Image
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayaeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo atangaze kuwa amepata watoto mapacha wawili, leo June 29 amepost picha akiwa na mapacha hao. Ronaldo ambaye timu yake ya taifa ya Ureno ambayo yeye ni nahodha wametolewa jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Chile, leo kuwaonesha hadharani watoto wake mapacha kwa kupost picha kwa mara ya kwanza.

Makosa matano wanayotuhumiwa Rais wa Simba SC na Makamu wake

Image
Simba SC Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kusikiliza mashitaka yao. Evans Aveva na Kaburu wameshtakiwa kwa makosa matano ambayo kwa mujibu ya sheria yanawanyima dhamana hivyo wamelazimika kwenda rumande hadi July 13 ambapo kesi yao itaendelea chini Hakimu Victoria Nongwa. Kutoka kulia ni Rais wa Simba Evans Aveva na wa pili kulia ni makamu wa Rais wa Simba Kaburu Makosa matano wanayotuhumiwa nayo viongozi wa Simba SC 1- March 5 2016 Evans Aveva anatuhumiwa kughushi nyaraka za kuidai Simba dola 300,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600. 2-March 16 zilitumika nyaraka za uongo kujilipa deni kupitia bank ya CRDB Azikiwe. 3- Kula njama na kutakatisha fedha kinyume cha sheria kiasi cha dola 300,000 za kimarekani. 4- Kosa la nne Evans Aveva anatuhumiwa kutakatisha fedha ambazo alizipokea kupitia bank ya Barclays tawi la Mikocheni. 5- Kaburu anatuhumiwa pia kumsaidia Evans Aveva kutaka...

Tabia Nne za Mpenzi Asiyekuwa na Penzi la Kweli.

Image
Ifahamikekuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi wmenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika mahusiano hayo hali ambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu kupenda. 1.      Muongo Hakuna asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika mapenzi uongo ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako hana penzi la dhati nawe na huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae endapo hautakuwa makini nae. Hivi karibuni nilikuwa mjini Mbeya nikipata chakula katika moja ya mgahawa uliopo mkabala na Posta, katika mgahawa huo nilikutana na vijana wawili na msichana mmoja wakiwa wanakula chakula ambapo kati ya kijana mmoja alionekana kuwa ni mpenzi mpya wa yule binti ambaye alisikika akisema kiwa ‘’ukija kwangu atakalia sofa ambazo hujawahi kuziona maishani’’ hali iliyonishtua na kuelewa mara moja kati ya tabia alizonazo kijana yule ambay...

STAR "SNURA" AWAASA WASANII CHIPUKUZI KUEPUKA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.

Image
Msanii wa muziki, Snura Mushi amewakanya vijana wanaotaka kuingia katika tasnia ya sanaa kuepuka vishawishi vya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya huku akidai kufanya hivyo hakufanyi uonekane unaenda na wakati. Snura amebainisha hayo baada ya kutuhumiwa akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinamfanya kumpa mizuka ya kufanya vizuri pindi akiwa stejini akitumbuiza. “Vijana wenzangu kama mnaingia kwenye sanaa achaneni na vishawishi, kuna vishawishi vya kipumbavu sana, eti uonekane unaenda na wakati na ndiyo vinawaponza watu wanaingia kwenye dawa za kulevya huko wanavuta bangi eti mtu apate stimu afanye kazi vizuri nani kakwambia?,” Snura alikiambia kipindi cha Enez cha EATV. “Mimi napanda kwenye steji situmii kilevi cha aina yeyote Mungu wangu aliyekuwa mbinguni ni shahidi sinywi pombe sivuti na nina panda kwenye steji nafanya vizuri tu kiasi kwamba wewe unaweza kufikiri nimetumia kilevi kwa sababu akili yangu nimeijenga kwamba hii ni kazi” aliongeza Snura. So...

Mfalme wa Saudia amfuta kazi mrithi wake.

Image
Mfalme Salman wa Saudia amebadilisha mkondo wa urithi na kumfanya mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman kuwa mwanamfalme na kuwa wa kwanza kumrithi. Aliyekuwa mwanamfalme Mohammed bin Nayef amepokonywa taji lake na kufutwa kazi kama waziri wa maswala ya ndani. Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa waziri wa ulinzi mbali na kuwa naibu waziri mkuu. Rais Bashir akataa kuonana na Trump Saudia Trump azuru Saudia, huku joto la kisiasa likimkabili nyumbani Mwanamfalme akatwa shingo Saudi Arabia Mabadiliko hayo yalitangazwa katika misururu ya amri za kifalme. Chombo cha habari cha Saudia kimesema kuwa mfalme ametaka raia wa taifa hilo kumtii mwanamfalme huyo mpya siku ya Jumatano. Hatua ya kumpa cheo hicho Salman iliidhinishhwa na wanachama 31 kati ya 34 wa baraza kuu. Wadadisi wanasema kuwa wale walio madarakani hupenda kuwateua watoto wao wa kiume kwa nafasi ambazo zitawawezesha kupandishwa vyeo. Mfalme Salman ambaye ni mtoto wa Mfalme Abdulaziz alishika hat...

MAGAZETINI LEO AL HAMIS JUNE 22 PATA HABARI KUU TOKA KURASA ZA MBELE NA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI KATIKA KURASA ZA NYUMA

Image