Makosa matano wanayotuhumiwa Rais wa Simba SC na Makamu wake


Simba SC Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu
walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kusikiliza mashitaka yao.
Evans Aveva na Kaburu wameshtakiwa kwa makosa matano ambayo kwa mujibu ya sheria yanawanyima dhamana hivyo wamelazimika kwenda rumande hadi July 13 ambapo kesi yao itaendelea chini Hakimu Victoria Nongwa.
Kutoka kulia ni Rais wa Simba Evans Aveva na wa pili kulia ni makamu wa Rais wa Simba Kaburu
Makosa matano wanayotuhumiwa nayo viongozi wa Simba SC
1- March 5 2016 Evans Aveva anatuhumiwa kughushi nyaraka za kuidai Simba dola 300,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600.
2-March 16 zilitumika nyaraka za uongo kujilipa deni kupitia bank ya CRDB Azikiwe.
3- Kula njama na kutakatisha fedha kinyume cha sheria kiasi cha dola 300,000 za kimarekani.
4- Kosa la nne Evans Aveva anatuhumiwa kutakatisha fedha ambazo alizipokea kupitia bank ya Barclays tawi la Mikocheni.
5- Kaburu anatuhumiwa pia kumsaidia
Evans Aveva kutakatisha fedha dola za kimarekani 300000 kupitia Bank ya Barclays tawi la Mikocheni.

Kwa mujibu wa sheria makosa ya kutakatisha fedha hayana dhamana hivyo Evans Aveva na Geofrey Nyange Kaburu watakuwa lumande hadi July 13.

Comments


Popular posts from this blog

Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini waimarika

harakati za ndesamburo na utajiri wake hizihapa

ACACIA wapinga vikali matokeo ya kamati ya pili ya Rais

IsraelIsrael yasalimu

mimi nipo sex Lulu diva

Real madrid mabingwa tena UEFA

Rais Zuma akiri kunusurika kuuawa kwa sumu

Hatua 10 Muhimi za Kumchagua Mchumba Mtakae Funga Ndo. a tzaama SOMA NA SHARE HII

Watu kumi na mmoja wauawa katika shambulio