STAR "SNURA" AWAASA WASANII CHIPUKUZI KUEPUKA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.


Msanii wa muziki, Snura Mushi amewakanya vijana wanaotaka kuingia katika tasnia ya sanaa kuepuka vishawishi vya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya huku akidai kufanya hivyo hakufanyi uonekane unaenda na wakati.
Snura amebainisha hayo baada ya kutuhumiwa akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinamfanya kumpa mizuka ya kufanya vizuri pindi akiwa stejini akitumbuiza.
“Vijana wenzangu kama mnaingia kwenye sanaa achaneni na vishawishi, kuna vishawishi vya kipumbavu sana, eti uonekane unaenda na wakati na ndiyo vinawaponza watu wanaingia kwenye dawa za kulevya huko wanavuta bangi eti mtu apate stimu afanye kazi vizuri nani kakwambia?,” Snura alikiambia kipindi cha Enez cha EATV.
“Mimi napanda kwenye steji situmii kilevi cha aina yeyote Mungu wangu aliyekuwa mbinguni ni shahidi sinywi pombe sivuti na nina panda kwenye steji nafanya vizuri tu kiasi kwamba wewe unaweza kufikiri nimetumia kilevi kwa sababu akili yangu nimeijenga kwamba hii ni kazi” aliongeza Snura.
Source:Bongo Newz

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC