hizi hapa sababu za Tundu lisu kutibiwa nairobi


Akitoa taarifa hiyo mara baada ya sala ya kuliombea bunge asubuhi ya leo ili kuanza vikao, Spika Ndugai amesema utaratibu wa matibabu kwa mbunge yeyote ulikuwa umeshafuatwa lakini familia iliamua yenyewe kumpeleka Nairobi, na siyo kama walishindwa kumpeleka nchini India.
"Baada ya bunge kupata taarifa kuhusu tatizo hilo, sisi bunge tulikuwa tumeshaagiza ndege tayari ilikuwa uwanjani, hapa Dodoma kwa ajili ya kumpeleka Hospitali ya Muhimbili ambapo ndiyo utaratibu wa kibunge, na kama kuna rufaa ya nje ya nchi utaratibu wetu ni kwamba serikali yetu ina mkataba na hospitali ya Apolo kule India, na ndiyo 'channel' ya sisi wote. Lakini kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni kwa sababu familia iliomba na Mh. Mbowe alieleza na mimi nilinukuu kwa niaba yake, walisema siyo kama wana mashaka na umahiri wa madaktari wetu, lakini wangejisikia faraja kwa wao wenyewe kuachagua kumpeleka kutibiwa Nairobi", alisema Spika Ndugai.
Spika Ndugai aliendelea kusema kwamba tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni la kwanza tangu historia ya bunge kuhamia Dodoma kwa miaka mingi, na kulivitaka vyombo vya dola kushughulikia tatizo hilo, huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu kwani hali yake inatia moyo.

Comments


Popular posts from this blog

Kubenea: Tundu Lissu anawajua kwa sura waliompiga risasi

W.C.B MARUFUKU NIGHT CLUB

Afariki kwakuchomwa na kisu

SUGU;:Tundu lissu ameniagiza niwaambie haya

Zitto aandika mazito kuhusu kifo cha Ndesamburo

DIAMOND HAKUNILIPA,” – SAIDA KAROLI

Man United kusajili nyota wapya watatu au wanne .