wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi
Watu wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi kati ya polisi na watu hao katika kijiji cha Ngnurunguru, kata ya Mandembo Tarafas ya Nampungu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi, polisi hao wakiwa katika majukumu mbalimbali ya ulinzi wa raia usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Nangurukuru walikutana na watu wakiwa kwenye pikipiki walijaribu kuwasimamisha walikaidi amri na kuanza kurusha risasi. Kamanda Mushi amesema kuwa polisi kwa kutumia mbinu za medani walifanikiwa kuwashinda watu na hao na kuwapiga risasi na kufa papo hapo, ambapo walikutwa na bunduki aina SR pamoja na risasi 41 zinazotumiaka na silaha hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi . Katika Tukio jingine Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbinga linamtafuta binti mmoja mwenye umri wa miaka 16 ambae jina lake limehifadhiwa kwa kosa la kutaka kumfukia mtoto wake mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa siku moja. Na Eatv
























Comments