MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kosa la kumvamia na  kumshambulia kwa mapanga Hakimu wa Mahakama  ya wilaya ya Masasi Halfani Saidi Ulaya na kumsababishia kifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Lukas Mkondya amesema hakimu huyo alivamiwa nyumbani kwake na watu watatu na kuanza kumshambua kwa mapanga sehemu za mikono na kichawani.

Hata hivyo Kamanda amesema baada ya kuhojiwa watuhumiwa hao wamekiri kushiriki tukio hilo la kumvamia Hakimu kwa lengo la kulipiza kisasi baada ya kuwahukumu wenzao kwenda jela kwa kosa la kufanya ujambazi na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Mtwara kutoa ushirikiano kwa wahalifu wa aina.


  Na ITV

Comments


Popular posts from this blog

wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi

Jumuiya ya Freemasons imetoa tahadhari nzito kwa Watanzania

Taarifa ya Serikali baada ya kauli za jana za Tundu Lissu

waziri mkuu majaliwa awa mkali

Kilichomkorofisha Mke wa Roma

. Ridhiwani Kikwete amefunguka haya kwa wananchi na baadhi ya viongozi wakae

Spika Ndugai Aagiza Kubenea Kusakwa, Zitto Kufikishwa Kwenye Kamati ya Maadili

Msigwa tunawindwa wabunge wanne CHADEMA -