Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC

Serikali ya Marekani juma hili imetishia kuwawekea vikwazo wale wote watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Kauli ya Marekani imekuja wakati huu mwishoni mwa juma lililopita mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, CENI Corneil Nangaa alitangaza kuwa tume yake haiwezi kuandaa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu.
Kuendelea kucheleweshwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa DRC huenda kukasababisha kuzuka kwa machafuko zaidi nchini humo ambapo katika maandamano ya mwaka jana mamia ya watu walipoteza maisha.
Naibu balozi wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa, Michele Sison amesema kuwa nchi yake iko tayari kutangaza vikwazo dhidi ya mtu au kundi la watu watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.
Nchi ya Marekani mwaka jana ilitangaza vikwazo kwa maofisa kadhaa wa juu wa Serikali ya DRC ikiwa ni pamoja na kuzuia mali na fedha zao na kuzuia raia wake kufanya biashara za watu waliowekewa vikwazo.
Hayo yakijiri shirika lisilokuwa la kiserikali linalotetea haki za binadamu la ACAJ nchini Jamhuri ya kimokrasia ya Congo limetoa wito wa kuachwa huru mara moja kwa wanaharakati wawili ambao walionyesha kupinga kauli ya tume huru ya uchaguzi CENI kuwa haiwezekani uchaguzi ufanyike mwaka huu wa 2017 nchini humo.

Na RFIRFI



Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee