Necta yatoa onyo kali.

Baraza hilo limewapa onyo wamiliki wa shule kuacha kuwaingilia wasimamizi wa mitihani hiyo kwakuwa shule zao ni vituo maalum vya kufanyia mtihani.
Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa (NECTA), Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandishi,amesema Baraza hilo linatoa wito kwa kwa wasimamizi wa mitihani wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu.
“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatua kali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa”
a mesema Dkt Msonde.
Amesema Baraza hilo linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi kuingilia majukumu ya wasimamizi.
“Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha Mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake wa unahatarisha Usalama wa Mitihani ya Taifa” amesema Dkt Msonde.
Hata hivyo, Dkt Msonde amesema Baraza hilo linaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri wanafunzi hao kwa kipindi cha miaka mine ya elimu ya sekondari hivyo hakutakuwepo na vitendo vya udanganyifu.
Pamoja na hayo, amesema katika mitihani huo jumla ya watahiniwa 585,938 wamesajiliwa kufanya mtihani huo, ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kujitegemea ni 62,425.
“Kati ya watahiniwa wa shule 323,513 waliosajiliwa ,wanaume ni 159.103 sawa na asilimia 49.18 na wanawake ni 164,410 sawa na asilimia 50.82,huku watahiniwa wenye uono hafifu ni 305 ambapo maandishi yao yanakuzwa”amesema Dkt Msonde.
Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa ni 62,425 ,wanaume ni 28,574 sawa na asilimia 45.77 na wanawake ni 33,851 sawa na asilimia 54.23 huku watahiniwa 6 wasioona.
Aidha, Baraza hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo ambayo inaanza kesho Oktoba 30 hadi 17 Novemba 2017 inafanyika kwa Amani na Utulivu huku akiwaomba wananchi hao kuheshimu eneo la mtihani linapofanyika.

Comments


Popular posts from this blog

wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi

waziri mkuu majaliwa awa mkali

Kilichomkorofisha Mke wa Roma

Msigwa tunawindwa wabunge wanne CHADEMA -

CHADEMA yafunguka Hospitali aliolaza Tundu Lissu

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

Anaandika Yericko_Nyerere

John Heche kuja na hoja binafsi muda wa Rais upunguzwe