Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alipoulizwa kuhusu uchaguzi huo, alisema watamtangaza mgombea wake, baada ya Nec kutangaza kuhusu uchaguzi huo. "Tutamtangaza mgombea wetu ambaye tutamsimamisha kwenye uchaguzi huo mdogo na tunaamini tutakayemsimamisha lazima atashinda," alisema Makene. Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima baada ya kuulizwa iwapo amekwishapata barua kutoka bungeni na lini itatangaza uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alifunguka na kudai kuwa muda ukifika watatoa taarifa. Kutangazwa kuwa wazi kwa jimbo hilo, sasa kunatoa fursa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza mchakato wa kupata mrithi wa Lazaro Nyalandu ambaye alitangaza kujizulu nafasi hiyo na kujitoa uanachama wa CCM mwanzoni mwa wiki. Taarifa iliyotolewa jana ilisema Spika wa Bunge, Job Ndugai, amemwandikia Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi. Taarifa ya Bunge ilisema Spika ameandika barua hiyo kwa mujibu wa ...