Posts

Kichuya asema yamoyoni

Image
Huu ni msimu wa pili, Kichuya kuwafunga Yanga, anasema anashukuru kuweka alama ya kumbukumbu kwenye mechi yenye ushindani kama hiyo ambayo mashabiki wanakuwa kwenye presha ya juu. " Binafsi siwezi hii ni kazi ya timu nzima na kufanikiwa kupata bao na wapinzani wetu wakaja kusawazisha kipindi cha pili,"

VPL; Ngoma ngumu

Image
Mtibwa Sugar imelazimishwa sare kye uwanja wake wa nyumbani hivyo kushindwa kukaa kileleni baada ya kufikisha alama 16 na kulingana na timu za Simba, Yanga na Azam FC. Mechi nyingine ni ile kati ya Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC ambapo Kagera Sugar imepata ushindi wake wa kwanza baada ya mechi 7, ikishinda mabao 2-1. Lipuli FC imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC. Njombe Mji ikiwa nyumbani imelazimishwa sare tasa na Stand United huku Majimaji ikitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC. Kesho kutakuwa na mchezo mmoja wa kukamilisha raundi ya nane kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu Shooting. Nafasi tano za juu kwenye msimamo zinashikiliwa na Simba yenye alama 16 ikifuatiwa na Yanga SC, Mtibwa Sugar na Azam FC zenye alama 16 pia. Singida United wanashika nafasi ya tano wakiwa na alama 13. Nafasi tatu za chini zinashikiliwa na Majimaji FC, Ruvu Shooting na Stand United zenye alama 5.

Necta yatoa onyo kali.

Image
Baraza hilo limewapa onyo wamiliki wa shule kuacha kuwaingilia wasimamizi wa mitihani hiyo kwakuwa shule zao ni vituo maalum vya kufanyia mtihani. Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa (NECTA), Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandishi,amesema Baraza hilo linatoa wito kwa kwa wasimamizi wa mitihani wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu. “Tunawaasa wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatua kali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa” a mesema Dkt Msonde. Amesema Baraza hilo linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi kuingilia majukumu ya wasimamizi. “Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha Mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake wa unahatarisha Usalama wa Mitihani ya Taifa” amesema Dkt Msonde. Hata hivyo, Dkt Msonde amesema Baraza hilo linaamini kuwa wal...

Polisi wawili wauwawa kwakupigwarisasi

Image
Polisi wawili waliokuwa kituo cha Polisi Kayole Nairobi wameuawa kwa kupigwa risasi na kisha wauaji kuondoka na bastola walizokuwa nazo Maafisa polisi wenzake kutoka kambi ya polisi ya Kirima waliikuta miili yao barabarani asubuhi. Mafisa hao wametambuliwa kuwa ni Konstebo Linus Inima and James Gitahi. Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga uchaguzi na eneo la Kayole huko Nairobi ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa na vurugu hizo, ila haijajulikana kama mauaji ya polisi hao yanahusiana na uchaguzi  Na jf

Simu ya marehemu ilitusaidia kunasa watuhumiwa

Image
Shahidi wa 11 wa upande wa mashtaka, koplo Seleman Faraji ameiambia Mahakama Kuu Kanda ya Moshi namna simu ya marehemu ilivyosaidia kuwakamata washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya. Akitoa ushahidi wake koplo Faraji ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa makosa ya kimtandao, alidai kuwa simu ya Msuya (marehemu) ilikutwa na ujumbe (SMS), uliomvuta kwenda eneo la tukio. Katika ushahidi wake huo alioutoa kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Lucy Kyusa shahidi huyo alidai kuwa katika kufanikisha mpango huo, zilisajiliwa namba mpya tano za simu kwa siku moja. Alidai Agosti 7, 2013, alikabidhiwa simu za marehemu aina ya Samsung Galaxy S4, iphone 5 na tablet moja kwa ajili ya uchunguzi na kufanikiwa kuondoa neno la siri kwenye simu ya iphone. Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kuondoa neno la siri, walibaini simu ya marehemu ilifanya mawasiliano na namba ya simu ya Airtel 0682 405323 ikimuelekeza Msuya kabla ya kifo chake, kwenda eneo la tukio. Katika uchunguzi huo, ...

Magazeti ya Tanzania leo Jumapili October 29, 2017

Image

Zitto Kabwe ametoa msimamo huu

Image
Chama cha ACT Wazalendo kimeziomba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia (WB) kufanya uchunguzi maalumu wa takwimu za kasi ya ukuaji wa uchumi ya robo ya pili ya mwaka na kuchukua hatua endapo itabainika kile anachodai kuwa Serikali ilipika takwimu. Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ametoa msimamo wake huo leo Jumamosi jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari. Zitto amedai chama hicho kimebaini takwimu zilizotolewa na Serikali za Aprili hadi Juni haziko sahihi. Amedai takwimu za Serikali zinaonyesha kasi ya ukuaji wa uchumi katika robo ya pili ya mwaka ni asilimia 5.7, tofauti na za ukokotozi kwa kanuni za kiuchumi anazodai zinaonyesha ni asilimia 0.1. "Hatujatafuta takwimu nyingine, hizi ni taarifa zilezile zilizotolewa na BoT na NBS lakini ukikokotoa utaona uchumi tulionao unasinyaa badala ya kukua na hali ikiendelea hivi hadi Juni 2018 kutakuwa hakuna uchumi Tanzania," amedai Zitto. Amedai sa...

Wabunge wanamna hii kufukuza ccm

Image
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi (CCM) Humphrey PolePole amesema kuwa mchakato wa kuwashughulikia viongozi mbalimbali ambao wanatuhuma mbalimbali umeanza na kusema wao watatenda haki kwa kuwapa nafasi ya kujieleza juu ya shtuma hizo au kashfa hizo na baadaye uongozi wa chama utafanya maamuzi juu ya watu hao. " Serikali hii imejikita kutetea na kusimamia haki na kuhakikisha uadilifu unasimamiwa na hakika haki itasimamiwa na mchakato mzuri wetu wa chama kuhakikisha kwamba mtu ameulizwa, amepewa tuhuma zake na amejitetea lakini sisi tunafanya uamuzi na tumeshakwisha anza kufanya uamuzi toka mwaka jana na mwaka huu katika vikao vinavyokuja na hakika Watanzania wawe na masikio tayari kuweza kujua na tutaendelea kudhihirishia Umma kuwa tunamaanisha kwenye mambo ya maadili" alisema Polepole Rais Magufuli aliwahi kumuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa Bungeni wanaweza kuwa utaratibu wao kuwaandikia viongozi wa vyama vya siasa juu ya wabunge mbalimbali ambao wanakuwa...

Magazeti ya Tanzania leo October 28 2017

Image
 Magazeti ya Tanzania leo October 28 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews