Hii ndiyo Nyumba aliyonunua Barack Obama
Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama amenunua nyumba ambayo kwa muda amekuwa akiishi pamoja na familia yake kwa kukodisha mjini Washington DC katika mtaa wa kifahari wa Kalorama.
Obama amenunua Nyumba hiyo yenye vyumba tisa ili kuendelea kukaa Washington na familia yake hadi binti yake mdogo, Sasha amalize masomo ya shule ya upili.



Comments