Popular posts from this blog
Nape Nnauye ameweka video ya Pius MsekwaMsekwa nakusema haya
Nape Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo itakuwa ni mingi sana. "Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya tulishafikiri na lilikataliwa kwa hiyo mimi na imani CCM itaendelea kulikataa hilo, tutabaki kwenye miaka mitano tu mara mbili basi" alisisitiza Msekwa Kufuatia kauli hiyo ndipo Nape Nnauye alipigiria msumari na kusema hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Mwalimu Julius Nyerer...
ubingwa wa dunia mikononi mwa Hamilton
Hata hivyo Hamilton ana nafasi ya kufanya hivyo baada ya kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye mpangilio wa magari wakati wa mbio hizo. Mkali huyo wa gia kutoka nchini Uingereza ameongoza mbio za kusaka nafasi kwenye kupanga magari ambapo sasa leo ataanza wa kwanza. Mpinzani wake wa karibu Sebastian Vettel kutoka timu ya Ferrari amemaliza wa pili hivyo gari yake itasimama kwenye nafasi ya pili wakati wa mbio za USGP leo akifuatiwa na gari ya Valtteri Bottas wa Mercedes ambaye atakuwa wa tatu. Mbio zitafanyika jioni ya leo kwenye mitaa ya Austin jijini Texas Marekani. Hadi sasa Lewis Hamilton anaongoza mbio hizo akiwa na alama 306 mbele ya Sebastian Vettel mwenye pointi 247. Baada ya mbio za leo za USGP zitakuwa zimebaki mbio 3 ili kumaliza msimu wa 2017 ambazo ni Mexico Grand Prix, Brazilian Grand Prix na Abu Dhabi Grand Prix.
mimi nipo sex Lulu diva
Muimbaji Lulu amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa alitambua kuwa yeye ni mzuri kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi kitu ambacho kilimfanya kutolaghaika na watu waliokuwa wakimsifia. “Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua,” amesema na kuongeza. “Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva. Hitmaker huyo wa Usimwache kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Utamu.
Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayaeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo atangaze kuwa amepata watoto mapacha wawili, leo June 29 amepost picha akiwa na mapacha hao. Ronaldo ambaye timu yake ya taifa ya Ureno ambayo yeye ni nahodha wametolewa jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Chile, leo kuwaonesha hadharani watoto wake mapacha kwa kupost picha kwa mara ya kwanza.
Mchawi wa Bongo Movie ni Sisi Wenyewe
Wengi wanamtambua kwa jila na Chausiku, lakini wazazi wake walimpa jina la Shamsa huku baba yake akijulikana kwa utambulisho wa Mzee Ford, hivyo si vibaya kama utamtambua kwa nomino ya Shamsa Ford, mama wa mtoto mmoja wa kiume, Terry. Hivi karibuni yalifanya mahojiano maalum na muigizaji huyu, nakualika tufuatane sote kweye aya zinazofuata hapa chini, kupata uhondo wa kile alichokisema. Swali: Kiasili wewe ni mwenyeji wa wapi? Shamsa: Mimi ni Mzaramo kwa upande wa mama na Mhehe kwa upande wa baba. Swali: Umezaliwa na kusomea wapi? Shamsa: Nimezaliwa na kusomea jijini Dar, hadi Kidato cha Nne lakini Kidato cha Tano na Sita nilisomea nchini Uganda ingawa sikubahatika kujiunga na masomo ya chuo kutokana na umasikini wa nyumbani kwetu (sauti ya kunywea kidogo). Swali: Unaishi na wazazi wako wote? Shamsa: Hapana, baba yangu alishafariki, alitangulia mbele za haki nikiwa mdogo sana, mwaka 2005, hivyo nimelelewa na mama lakini namshukuru Mungu maana yote ni kwa mapenzi yake. Swali:...
TETESI ZA SOKA ULAYA LEO
Manchester United wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa Tottenham Danny Rose,27, mwezi Januari (Tuttomercato, via Talksport) Barcelona wanajitahidi kumpata mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, kwa pauni milioni 89 kabla ya thamani ya mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 kupanda msimu ujao (Mundo Deportivo, via Daily Mirror) Paris St-Germain wako katika mikakati ya kumuuza wing'a Angel di Maria, 29, kwenda China mwezi Januari.(TMW, via Sun) Arsenal wameafikia makubaliano na wing'a wa zamani Marc Overmars,44, ya yeye kuondoka Ajax na kuwa mkurugezi wa kandanda kuanzia msimu ujao.(Tuttomercato, via Daily Express) Mchezaji wa kiungo cha kati wa zamani wa Italia Andrea Pirlo, 38, hajakana mpango wa kujiunga na kikosi cha makocha, kufuatia uamuzi wake wa kustaafu misho wa msimu wa MLS. (Gazzetta dello Sport, via London Evening Standard) Meneja wa Manchetser United Jose Mourinho alikuwa ndani umati wakati wa ushindi wa Austria dhidi ya Serbia, kumtazama wing'a w...
Hii ndiyo Nyumba aliyonunua Barack Obama
Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama amenunua nyumba ambayo kwa muda amekuwa akiishi pamoja na familia yake kwa kukodisha mjini Washington DC katika mtaa wa kifahari wa Kalorama. Obama amenunua Nyumba hiyo yenye vyumba tisa ili kuendelea kukaa Washington na familia yake hadi binti yake mdogo, Sasha amalize masomo ya shule ya upili.
, Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na baadhi ya mawakili wanaounga mkono wito uliotolewa na Tundu Lissu wa kuwataka mawakili wote kugomea kufika Mahakamani kutekeleza majukumu yao ya kisheria ikiwa ni kuonyesha msimamo wao wa kupinga kitendo cha jengo la mawakili wa IMMA kulipuliwa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni bomu la petroli. Hata hivyo, wito huo haukuitikiwa na mawakili wengi kama ilivyotarajiwa na Tundu Lissu kwani wengi walifika kusikiliza kesi zinazowahusu katika mahakama mbalimbali nchini. "Sio kwamba sisi hatujaguswa na kilichowapata wenzetu wa IMMA Advocates isipokuwa hili la Rais wao Tundu Lissu ni kuchanganya mambo mawili yasiyohusiana kwani kuchomwa kwa ofisi tayari Polisi wanafanya uchunguzi na hawajatoa majibu na hiyo ni Taasisi iliyo chini ya Serikali ambapo Mahakama ni mhimili unaojitegemea hauingiliani kimajukumu...
msuva ageuka lulu dau la usajili lapanda hadi........
Msuva amejiunga na timu hiyo Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga, lakini sasa ukitaka kumpata, Waarabu wanamthaminisha kwa euro 475,000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3. Mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao sita kwenye ligi ya nchi hiyo huku akifunga mabao manne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali ya mabao hayo, Msuva amefanikiwa kucheza mechi 16 za ligi na moja ikiwa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliofanya thamani yake kuongezeka. Kwa mujibu wa mtandao mmoja maarufu nchini Morocco ambao unahusika kutoa taarifa za thamani ya wachezaji, dau la Msuva sasa ni euro 475,000. Dau hilo ambalo limeonekana kupanda kwa Msuva, pia unaweza kusajili kikosi kizima cha Simba ambacho kilitajwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 1.3. Kuongezeka kwa thamani ya mshambuliaji huyo, kumetokana na kuonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi ya Morocco tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Yanga msimu uliopita ambao aliondoka akiwa ni mfungaj...




























Comments