Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 18 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa
Liverpool watapambana na Hoffenheim ya Ujerumani ili kufuzu kucheza ngazi ya makundi ya UEFA Klabu Bingwa Ulaya. Liverpool watacheza ugenini duru ya kwanza Agosti 15 au 16, na marudiano Anfield Agosti 22 au 23. Washindi 10 katika mechi hizo za kufuzu wataungana na timu 22 ambazo tayari zimefuzu kucheza ngazi ya makundi ya Uefa Champions League. Mechi nyingine ni kama ifuatavyo: Sporting Lisbon (Portugal) v Steaua Bucharest (Romania) Hoffenheim (Germany) v LIVERPOOL (England) Napoli (Italy) v Nice (France) Young Boys (Switzerland) v CSKA Moscow (Russia) Istanbul Basaksehir (Turkey) v Sevilla (Spain) Hapoel Beer-Sheva (Israel) v NK Maribor (Slovenia) CELTIC (Scotland) v Astana (Kazakhstan) Olympiacos (Greece) v NK Rijeka (Croatia) APOEL Nicosia (Cyprus) v Slavia Prague (Czech Republic) Qarabag FK (Azerbaijan) v Copenhagen (Denmark)
Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliyoijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma imeungua moto jioni hii. Nyumba hiyo iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa imeteketea yote na chanzo chake hakijafahamika hadi sasa. Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata hivyo Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo. Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua ilikuwa ikitumika kwa dharura.
Mamiloni ya wanawake nchini India hawajawai kuwaita mabwana zao kwa kwa majina yao ikiwa ni njia ya kuwaheshimu. Tamaduni hiyo inaheshimika zaidi vijijhini licha kutokuwepo saana mijini. Sasa waendesha kampeni wanawashauri wanawake vijijini paia nao waachane na tamaduni hiyo. "Wazazi wangu walioana kwa miaka 73 hadi babangu alipoaga dunia mwaka uliopita. Na bbc
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayaeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo atangaze kuwa amepata watoto mapacha wawili, leo June 29 amepost picha akiwa na mapacha hao. Ronaldo ambaye timu yake ya taifa ya Ureno ambayo yeye ni nahodha wametolewa jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Chile, leo kuwaonesha hadharani watoto wake mapacha kwa kupost picha kwa mara ya kwanza.
Real Madrid wamewaambia Manchester United kuwa ikiwa wanahitaji kumsaini Gareth Bale 28, watalazimika kumuachia kipa David de Gea 26, ili ahamie Bernabeu. (Mirror) Meneja wa zamani wa Livepool Rafa Benitez huenda akahama Newcastle kujiunga na Everton ikiwa Ronald Koeman ataihama Everton. (The Sun) Mesut Ozil 28, na Alexis Sanchez wote wa Arsenal hawatakuwa na mikataba miwishoni mwa msimu na Arsenal inatakata kuwauza mwezi Januari. (Star) Itawalazimu Liverpool na Barcelona kumng'ang'ania mlinzi wa Southampton Virgil van Dijik, ikiwa wangependa kumsaini mwezi Januari. (Mirror) Everton wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 31 kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon, William Carvalho 25, licha ya klabu hiyo ya Ureno kusema kuwa haumuuzi. (Daily Mail, via Record) Mshambuliaji wa Everton Henry Onyekuru 20, amethibitisha kuwa alikutana na maafisa wa klabu yake wiki iliyopita kuzungumzia kurejea mapema kutoka kwa mkopo na klabu ya Anderlecht. (Liverpool Echo) Ars
KAMPALA: Katikati ya majonzi, yapata siku 15 tu tangu mumewe, Ivan Ssemwaga ‘Ivan Don’ azikwe huko Nakalilo nchini Uganda baada ya kufariki dunia ghafla, aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, anadaiwa kuwatibua Waganda kufuatia kushiriki matukio matano (5) yanayotafsiriwa kuwa ni ya aibu, Amani linayo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya udaku nchini Uganda, tofauti na ilivyotarajiwa, kama ilivyo kwa baadhi ya tamaduni za Kiafrika, kuwa Zari angekuwa kwenye maombolezo kwa siku arobaini au hadi amalize eda kwa kufi wa na mume huyo, yeye amekuwa akijihusisha na ishu ambazo zinaacha watu midomo wazi. AIBU YA KWANZA Ilielezwa kwamba, siku mbili tu baada ya mazishi ya Ivan, Mei 30, mwaka huu, Zari alitupia video kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ikimuonesha mwenye furaha tele huku akikata mauno ya hatari hivyo kushangaza wengi walioamini ni video ya zamani. Ilisemekana kuwa, ili kuonesha video hiyo haikuwa ya zamani, Zari aliambatanisha na maneno ya
Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 21 2017 kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.
Mchungaji Peter Msigwa amesema hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea vizuri na anatamani apate nafuu na kunyoosha vidole viwili (ishara ambayo hutumiwa na Chadema). Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum leo Jumatano jioni jijini Dar es Salaam, Mchungaji Msigwa amesema kwa kipindi chote hicho Lissu hakuwa akila na hali yake imebadilika ukilinganisha na alivyokuwa hapo awali lakini hivi sasa anakula vitu laini. kabla sijaanza safari ya kuja (kurudi Dar es Salaam) amenitania sana kwa kusema anatamani apate nafuu na kuonyesha alama ya vidole viwili,” amesema Mchungaji Msigwa. Msigwa ameeleza wanaendelea kujadiliana na madaktari ili kuangalia uwezekano wa kumpeleka nchi nyingine kwa ajili ya matibabu zaidi. Amesema Lissu anaangaliwa na madaktari 10 kila mmoja akishughulika na eneo lake ili kuhakikisha hali yake inatengemaa. “Miongoni mwa mambo anayoyarudia ni kututaka kuendelea kupambana, kupaza sauti kuikomboa nchi, ”amesema Msigwa.
BAADA ya mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kusambaza kitabu alichokipa jina la Siri za Flora Mbasha kilichoanika ‘mabaya’ ya aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, mumewe huyo ameibuka na ‘kumchana’ vibaya mwimbaji huyo na kusema hafai kuwa mke. Flora alikiachia kitabu hicho hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliyopitia kwenye maisha yake na Mbasha, alieleza namna ambavyo mumewe huyo wa zamani alivyokuwa akimtesa na hata kumuingilia kwa nguvu akiwa kwenye siku zake. Akizungumza na mwanahabari wetu katika ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, Mbasha alianza kwa kueleza masikitiko yake juu ya kitabu hicho kwa kusema anashindwa kuelewa mume wa sasa wa Flora, Daud Kusekwa anajisikiaje pale Flora anapomzungumzia mara kwa mara. “Yaani unajua watu wengine sijui wapoje bwana. Hivi kweli wewe hata huyo mwanaume wake anajisikiaje kuona mkewe ananiongelea kila wakati? Ni kukosa adabu, kwa nini wasifanye maisha yao? “Kweli mwanamke aliyefunzwa, akafunzika
Comments