mengine yasemwa tarime

Y
Mara Ryoba amesema kuwa polisi wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu wa CCM wakiendelea kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali watu wa upinzani wakizuiliwa.
"Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh. John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu" alisema Mbunge Marwa Ryoba
Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne.
"Ni kweli polisi walitaka kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.


N

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .