messi aamua kutokuwa mbinafsi

'
'Nafikiri nimekua, kwasasa sichezi sana peke yangu japo nakimbia kwenye njia zangu lakini najitahidi kucheza na wenzangu, natamani timu icheze zaidi katika maeneo yote ndio mana nakuwa mchezeshaji mzuri'', amesema Messi kwenye mahojiano na Runinga moja.
Messi amekuwa na msimu mzuri ambapo hadi saa amefunga mabao 34 kwenye michuano yote msimu huu huku akifunga mabao matatu kwenye ushindi wa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa UEFA hatua ya 16 bora wiki iliyopita.
Alipoulizwa kuhusu kumsaidia nyota mpya wa timu hiyo Ousmane Dembele Messi alijibu kuwa yeye anasaidia timu ambayo inawachezaji 10 na yeye wa 11 hivyo msaada wake unaweza kwenda kwa yoyote japo amekiri kufurahia namna ambavyo Dembele anajituma uwanjani.
Messi kesho atakuwa uwanjani kuiongoza timu yake kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Athletic Bilbao huku wakitaka kulinda tofauti ya alama 8 waliyonayo na timu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili.

Comments


Popular posts from this blog

mimi nipo sex Lulu diva

Tabia Nne za Mpenzi Asiyekuwa na Penzi la Kweli.

Wsanii wanaowania MTV Europe Music Awards

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

IsraelIsrael yasalimu

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu mikononi mwa polisi