TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

Arsenal wanafanya jaribio la dakika za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Julian Draxler, 23, na wakimkosa watazuia uhamisho wa Alexis Sanchez, 28, kwenda Manchester City. (Daily Mirror) Manchester City watapanda dau la pauni milioni 70 taslimu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, na tayari wamepeleka kikosi chake cha wansheria na madaktari nchini Chile kwa ajili ya kukamilisha usajili huo. (Independent) Matumaini ya Manchester City ya kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, bado ni ati ati, kwa sababu Eliaquim Mangala, 26, ambaye angehusika katika mkataba huo hataki kwenda West Brom. Arsenal na Leicester walipanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki huyo, lakini maombi yao yalikataliwa. (Daily Telegraph) Crystal palace wana matumaini ya kumsajili Eliaquim Mangala kutoka City kwa pauni milioni 23. (Sun) Swansea wanakaribia kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches kwa mkopo. (Guardian) West Ham wanapanga kumchu...