Meneja wa tume ya uchaguzi aliyetoweka Kenya apatikana amefariki

Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki. Mwili wa Christopher Chege Musando, ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi wa masuala ya teknolojia wa IEBC, umepatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti jijini Nairobi Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake. Na BBC