HAKIMU AJITOA KESI YA MBUNGE GODBLESS LEMA.

Hakimu mmoja anayesikiliza kesi za Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amejitoa katika kusikiliza kesi ya kiongozi huyo ambapo baadhi zinatarajiwa kuanza kuunguruma Juni 20 mwaka huu baada ya upelelezi kukamilika. Hakimu amesema kuwa, kiongozi huyo ana jumla ya mshataka manne ya uchochezi ambayo yote yapo mikononi mwake, ndio sababu ameamua kujitoa kusikiliza moja ya mashtaka hayo. Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi Desderi Kamugisha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alifafanua amefikio uamuzi huo baada ya kuona si busara kesi zote hizo kuwa mikononi mwake. Hakimu Kamugisha amejitoa katika kesi ya jinai namba 441/2016 ambayo Lema anadaiwa kutoa matamshi ya kumkashifu Rais Dkt Magufuli Oktoba 23, mwaka jana wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa. “Kiburi cha Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake. Rais ni mbabe na watu anawaonea, wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyab...